Je ni vipi naweza kutengeneza App yangu kama sina uelewa wa hizo lugha(Codes)

 

Huu ni mfano wa simple app iliyotengenezwa na Andromo


*Leo tujifunze namna ya kutengeneza Apps bila kua na uelewa wowote ule wa codes*

(simple apps)

Unaweza kutengeneza app na kupata faida kama nilivyokueleza mwanzo. Mfano kama wewe unamiliki blog au website(nitazizungumzia baadae na kujua faida zake) na unahitaji kuzibadili na kua app basi usiogope ni rahisi sana, kuna software ambazo zinatumika kubuild Apps bila ya kutumia Codes. Inamaanisha wewe utakua tu una add kitu unachokitaka *Nb vitu vyote vinakua tayar vipo wewe kazi yako ni kuvipangilia tu.

Pia software za kulipia ndio zinaweza kutengeneza app zenye mvuto zaidi na utapewa option ya kumonetize app yako na kuweza kupata pesa

Mojawapo wa software nzuri kabisa za app ni website ya Andromo(www.andromo.com)

Website hii inakupa option ya kulipia au kutengeneza bure. Na ni rahisi tu kutumia website hii

1. unajisajili kupitia www.Andromo.com

2. Watakutumia email na itatakiwa ucomfirm

3. Utaanza kutengeneza app na kubuild Apk


Pia kuna website inaitwa Kodular website hii ni nzuri zaidi maana inakupa option ya kutengeneza kawaida na pia unaweza kutumia codes kutengeneza apps zako

Pia kuna baadhi ya apps ambazo zinapatikana playstore nazo zinakuruhusu wewe mtumiaji kutengeneza apps na apps hizo ni kama vile

1. App builder

2. Apk builder

3. Web2apk builder n.k


Ila ningependa kuwashauri kwanza endapo unataka kutengeneza app kupitia software hizo basi inakubidi uwe na website au blog ili app yako iwe ni dyanmic yaan uwe na uwezo wa kupost kitu na watumiaji wa app yako wakakisoma hicho kitu. Maana kama itakua Static inamaana kama umeandika habari basi itakua ni hiyo hiyo ukitaka kuibadili ni mpaka utengeneze app mpya sasa hiyo itakupotezea muda. Ningependa kulirudia somo la Blog ili iwe ni rahisi watu kutengeneza Apps zao.

Somo lijalo unatengeneza vipi blogs.

Comments

Post a Comment