Jinsi/namna ya kutengeneza pesa mtandaoni kwa kumiliki Mobile Apps

 



Kuna njia nyingi za kutengeneza pesa mtandaoni kama vile kufupisha links na kusambaza,kuanzia blogs na websites,kutengeneza mobile apps,kutengeneza software mbalimbali,pia kuna kazi kama vile freelancer ambazo unaweza kuzifanya mfano kama kudesign invitation cards,id cards n.k ambapo unaweza kujisajili kupitia fiverr.com na kuna makampuni mengine mengi(ntatuma link) ambapo utakua unachagua kazi unayoiweza unaifanya na kupokea malipo yako..pia unaweza kuanzisha youtube channell,kuuza bidhaa mbali mbali mtandaoni n.k


Tutazizungumzia njia moja moja na leo tunaanza na utengenezaji wa Mobile apps(Android apps na Ios Apps), 

1.mobile apps ni nini?

Mobile apps ni programu ambazo zinaweza kufanya kazi kwenye simu kama vile games,chatting apps na kadhalika...soko la mobile apps limekua sana duniani pia ni moja ya soko ambalo linalipa sana. mfano mzuri wa mobile apps ni kama vile Whatsapp,instagram,tiktok pia kuna apps za biashara kama vile Kikuu,Alibaba,Aliexpress n.k 

2.je ushawahi kujiuliza ni faida kiasi gani wanayopata wamiliki wa Mobile Apps?

Wamiliki wa Apps hizi wanapata faida kubwa sana,makampuni makubwa kama Facebook wanaingiza zaidi us dollar bilion 20 kwa mwaka na takribani dollar milioni moja kwa wiki.hivyo basi ni soko ambalo linalipa sana kama utawekeza vizuri.matajiri wakubwa kama vile jeff bezos,Bill gates bila kusahau mmiliki wa Facebook company ambayo ni wamiliki wa instagram na WhatsApp..Mark Zuckerburg.pia tusisahau wamiliki wa Google ambao ni Sergey brinn na Larry Page ni mojawapo ya watu wanaongiza mkwanza mrefu sana kutokana na kumiliki na kuziendesha vizuri mobile apps zao na pia wote hao niliowataja hapo wanaonekana katika Top 10 ya matajiri duniani

3. Je wanapate faida kupitia Apps hizo?.

Katika Apps kuna kupata faida kwa njia takriban mbili ambazo ni Ads(Matangazo) na inApp purcahse(mauzo ya ndani ya Apps)


4. Wanapataje faida kupitia matangazo(Ads)?.


Katika apps huwa kunakua na matangazo ya aina kadhalika mfano google ads na facebook ads, pia kuna makampuni mengine ya matangazo kama vile StartApp n.k ila yajulikanayo sana ni hayo mawili Facebook na Google.

Mfano mzuri ni kua, kama wewe unahitaji kutangaza tangazo zako instagram or facebook itakulazimu ulipie mfano facebook ni 5$ = 12,000 kwa siku hivyo basi fikiria kama kwa siku watu zaidi ya 2million ambao ni watumiaji wa facebook watapost matangazo yao itakua ni zaidi ya 1.5$ Billion ambayo kwa pesa zetu tanzania ni zaidi ya matrilioni pia fikiria kwa siku moja ni 5$ na kwa siku saba 35$ na kama user zaidi ya 2million wakaweka matangazo yao je atapata faida kiasi gani????

Hivyo hata wewe ndugu msomaji unaweza ukatengeneza app ambayo watu wakitaka kupost tangazo ni lazima wa lipie hata kama utaweka 1$ per day bado utapata faida nzuri tu.


5. Je utapata faida vipi kama app yako sio ya kupost matangazo??


Bado utapata faida hata kama app yako haikuruhusu kupost matangazo.mfano umetengeneza App ya Whatsapp status saver bado utapata faida kupitia matangazo na hii inatokana kwa makampuni kama vile google ads na facebook ads. nk mfano mzuri ushawah kufungua App na ukakuta ghafla tangazo limetokea au ghafla kuna video ya tangazo imetokea alaf inakupa option ya kukata...ndio pesa ile.

Je inapatikana vipi pesa pale?

Kama nilivyotangulia kusema kuna makampuni kama google na facebook wao wanaruhusu kuweka matangazo yao katika Apps zako. Mfano wa matangazo hayo kuna aina kama 4 hivi nazo ni

1. Banner ads 2. Native ads 3. Reward ads na 4. Interestial ads 

Na kila aina ya tangazo hapo ina range ya pesa yake hivyo basi baada ya wewe kutengeneza App yako utawaomba google or facebook na watakuwezesha kuweka matangazo katika apps zako na watakulipa vizuri. 

Je pesa inatokana vipi na matangazo hayo?

Pesa inapatikana pale ambapo app yako itakua na watumiaji wengi mfano katika app yako ya kudowaload status za whatsapp ukaweka matangazo na app yako ikawa na watumiaji zaidi ya 1000 inamaana kila akifungua na kutumia app hiyo atakutana na tangazo hivyo basi tufanye 1 click ya kukata tangazo ni 0.001$ na kwa siku watu zaidi ya 1000 wakatumia hiyo app yako basi utatengeneza sio chini ya 10$ ambayo ni sio chini ya 25,000 Tzshillings pia fedha hizo zinatokana na aina ya matangazo uliyoweka kama ni banner au reward basi pesa itakua ni tofauti.

 5. Aina za matangazo(banner,reward,interestial na native)


Aina hizi hulipa kutokana na tangazo mfano mzuri kwa watumiaji wa apps mbali mbali mshawah kukutana na vimatangazo ambavyo huwa vinakua upande wa chini ya app or juu vinakuaga vyembamba..sasa aina hiyo ya matangazo inaitwa Banner.

1. Banner ads

Haya ni matangazo ambayo huwa yanatokea upande wa chini au juu wa aps yako pia ni membamba kimuonekano. Na pia matangazo haya ndio hupendelewa zaidi na developrs wengi kuyaweka katika apps zao japo hayalipi pesa nzuri tofauti na mengine. Faida moja wapo ya matangazo haya huwa hayaleti usumbufu kwa watumiaji wa apps na ndio maana hupendelewa zaidi


2. Interestial ads

Aina hii ya matangazo hutokea full screen..Matangazo haya pia hupendelewa na watu kwa sababu huwa linatokea tu ghafla na kukupa option ya kulikata pia ni moja ya matangazo ambayo hulipa pesa nzuri tofauti na Banner ads.


Mfano wa interestial ads


3. Native Ads

Haya ni matangazo ambayo huwa mixed video na picha pia matangazo haya hutokea ghafla labda kama unaingia kwenye app or unataka kuext na kadhalika.

Matangazo hawa hatutumii sana kwa sababu husumbua watumiaji wa apps. Japo ni moja ya matangazo ambayo hulipa vizuri zaidi ya Banner na Interestial.


4. Rewarded ads

Aina hii ya matangazo hupendelewa zaidi kuwekwa kwenye games. Nafikiri umeshawah kucheza game labda la magari na baada ya gari lako kuishiwa mafuta na huna coin za kununua mafuta basi wanakupa option ya play video ad to get fuell or coin na ukigusa hapo ghafla itatokea video fupi isiozidi sek 30 na kuiangalia yote na baada ya hapo unakuta gari imejaa mafuta au wamekupa coin. Sasa aina hii ya matangazo ndio Rewarded Ads 


 Picha ya aina za matangazo za google.

Matangazo haya ndio hulipa vizuri zaidi kuliko. Matangazo yote.

*NB. Unapoweka matangazo usiangalie zaidi katika kupata pesa angalia pia usiwasumbue watumiaji maana hawapendi apps zenye matangazo mengi.

*Facebook ads ndio kampuni inayolipa vizuri na hawana mashart mengi kama Google ads*

6. Kupata pesa kwa njia ya InApp purchase.

Nafikiri mshawahi kutumia apps ambazo inabidi uingize credit card yako ya bank na kununua coin ili uweze kutumia apps hizo na hii ni mara nyingi hutokea kwenye Games mfano game la magari ukaishiwa mafuta na huna coin basi watakupa option ya kuangalia reward ads or watakwambia ununue coin kwa kupitia pesa yako(pesa halali) ambapo itakubidi uingize taarifa za kadi yako ya bank na kulipia kiwango hicho cha pesa.


Hivyo basi unaweza ukaamua leo ukapata wazo na kutengeneza apps zako ambazo itakua ni uhakika kupata pesa na pia kumbuka wazo zuri na app yenye ubora ndio itavutia watu zaidi na kuitumia.

*NB. Kama huna uwezo wa kutengeneza Apps itakubidi umuajiri developer kwa kazi hiyo ila kama unauwezo basi andaa wazo na kutengeneza kitu kilicho bora


Unaweza kuniajiri pia kama developer tuma email ya maelezo kwenye

Blmcompany20@gmail.com

Whatsapp number:+255626653295

Pia nitaandaa somo la kutengeneza apps ambalo litakua live kupitia Youtube.pia mnaweza kupendekeza njia nyingine.


Asante.

Comments