1. Blogs ni nini?
Blog ni aina ya website ambayo huwa inakua chini ya makampuni maalumu kama vile google n.k
Ni rahisi sana kutengeneza blog na kama utafanikiwa kufuata sheria zao na mashart basi utaanza kulipwa kama wamiliki wa Apps.
2. Hatua za kutengeneza Blog.
1.unafungua browser yako na kutafuta www.blogger.com
2.watakwambia uingize email na password yako kama kifaa chako hakikua na email( kumbuka kutunza Email na password yako maana hizi ndio funguo zitakazokuruhusu wewe kuingia katika blog yako na kupost habari.
3. Utaandika link ambayo ungependa blog yako iitwe mfano hii ni. Www.jifunzetech.blogspot.com Hapa kumbuka inatakiwa utumie jina unique pia ni vizuri zaidi kama jina lako litakua fupi na lakueleweka litakua ni rahisi zaidi kutafutwa.
Pia unaweza kuweka custom domain name kama tayar uliinunua. Na hizi huanzia 2$ na kuendelea mfano wa custom domain ni www.jifunzetech.com au www.jifunzetech.org pia www.jifunzetech.co.tz na pia domain hizi unaweza kuzinunua kwenye makampuni kama vile godady,iFast na pia kampuni la bei rahisi ni Namesilo ila kama unahitaji domain za kitanzania unaweza kunitafuta nikakupa maelekezo ya kuzipata. Mfano wa domain za tanzania ni www.jifunzetech.co.tz hilo neno .co.tz ndio custom na huwa linalipiwa kila mwaka.
3. Baada ya hapo utaandika jina la Blog yako mfano hii inaitwa JIFUNZETECH hivyo wewe utaandika jina utakalopenda
4.mpka hapa blogu yako itakua tayari imekamilika. Na utaweza kupost habari, picha , videos n.k pia utaweza kuiboresha zaidi kwa kununua Themes skin yaani muonekano ila sio lazima .
Je? Tunapataje pesa kutumia hizi Blogs.
Kama nilivyotangulia kuwajuza kua huwa kunakua na njia mbili za kuingiza pesa ambazo ni kuuza matangazo na pia kuweka matangazo(Katika blogs za blogger hatuwezi weka matangazo ya facebook huku tutatumia Google Adesense)
1. Utapataje pesa kupitia kuuza matangazo?
Ni rahisi tu, mfano wewe katika blog yako inatembelewa na kusomwa na watu zaidi ya 5000 kwa siku basi kama kuna mtu anataka kutangaza biashara au bidhaa au tangazo lolote lile basi atakuona na mkaelewana bei mfano. Tangazo moja ukaweka kwa 2500/=Tzs kwa siku inamaana mtu akitaka kuweka kwa wiki basi ni 17,000/=Tzs na utazidi kupata faida endapo blog yako itasomwa na wengi zaidi na makampuni na watu binafsi watakupa matangazo yao na kuposti huko
2. Utapataje pesa kupitia Google Adesense
Ili kiweza kupata pesa kupitia google adesense basi itakulazimu uwe umekidhi vigezo na masharti ya google na mojawapo ya mashart makuu ni kua
A. Hutakiwi kukopy habari kutoka katika blog ya mwenzako na kuweka kwako.
B. Inatakiwa uwe na post zaidi ya 10.
C. Itapendeza zaidi kama utatumia custom domain
Endapo utafanikiwa kukidhi. Vigezo hivyo basi utafanikiwa kupewa ruhusa ya kuweka matangazo ya Google.
Ambapo ukiweka matangazo na blogs yako ikasomwa zaidi ya watu 500 kwa siku basi hutokosa 2$-5$ mpka 10$ sasa fikiria kiasi hicho ni kwa siku je ukiingiza kwa mwezi itakua ni bei gani..
Na pia kumbuka katika kazi hizi inahitajika uwekeze muda wako pia uwe active ili watu waweze kupata new habari kila wanapotembelea blog yako.
* Somo lijalo ni jinsi ya kuweka matangazo katika blogs na Apps zako.
Comments
Post a Comment